Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 10:44 pm

NEWS: SERIKALI YAWATOA HOFU WAWEKEZAJI WA MADINI NCHINI

DODOMA: SERIKALI imewatoa hofu wawekezaji waliopo katika sekta ya madininchini na kwamba haitawabughudhi katika uzalishaji wao wa madini hivyo wawe watulivu na kuwataka kuendelea na kazi zao.

Kaulli hiyo imetolewa leo Bungeni Mjini Dodoma na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,KASSIM MAJALIWA wakati akijibu swali la Mbunge wa Tabora, EMMANUE L MWAKASAKA katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa waziri Mkuu.


Mbunge huyo alitaka kujua nini tamko la Serikali, baada ya kuzuia michanga ya dhahabu kwenda nje ya nchi na kwamba haioni itakuwa na mahusiano mabaya na nchi mbalimbali Duniani pamoja na kuwepo kwa athari Za kiuchumi.

Akijibu swali hilo, Amebainisha kuwa lengo la Serikali kuzia mchanga wa madini kwenda nje ya nchi ni kwaajili ya kujiridhisha kuwa mchanga huo una nini.


Hata hivyo amesema kuwa kwa sasa Serikali ipo katika matarajio ya kupata taarifa ya pili ambayo itawashirikisha wataalam mbalimbali wakiwemo wa kisheria toka sekta mbalimbali kuona hatua gani za kuweza kuchukua.