Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 10:37 pm

NEWS: SERIKALI YAWATAKA WAKANDARASI KULIPA TOZO ZA SERIKALI ZA MITAA

DODOMA: SERIKALI imewataka Wakandarasi wote nchini kuanza kulipa tozo za Serikali za mitaa yaasilimia 0.3 kwa mujibu wa Sheria pamoja na kushiriki katika shughuli za maendeleo kwani ni takwa la Kisheria.

Pia imewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuyataka Makampuni yanayochimba Kokoto na Mchanga kuanza kutoa ushuru katika Serikali za mitaa ili wananchi na Taifa kwa ujumla waweze kunufaika.

Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Nishati na Madini,MEDARD KALEMANI wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mkuranga,ABDALLAH ULEGA.

Mbunge huyo alitaka kujua kama wananchi wa maeneo ya Mkuranga wananufaika na madini yaliyopo katika eneo hilo hasa mchanga kutokana na kuwepo kwa wawekezaji, na ni lini Gesi itaanza kutumika katika eneo la Mkuranga hasa Kiparang’anda.

KALEMANI amefafanua kuwa shughuli zinazo fanyika sasa katika eneo la Kiparang’anda ni ukamilishaji wa utafiti wa madini ya gesi asilia ambapo Gesi katika eneo hilo itaanza kutumika Agosti mwakani ambapo maeneo ya kiparanganda,pwani na Dar-es-Salaam pamoja na maeneo mengine watanufaika na gesi hiyo.

Pia katika swali la msingi Mbunge ULEGA alitaka kujua kama Serikali inafahamu kuwepo kwa madini katika ukanda wa Pwani ya Tanzaniaambapo Serikali imekiri kuwepo kwa madini mbalimbali katika ukanda huo.