- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SERIKALI YAWATAKA KAMATI YA MISITU KUONGEZA JUHUDI
DODOMA: SERIKALI imeitaka kamati ya kitaifa ya ushauri wa masuala ya misitu nchini kusaidia kuongeza juhudi za kulinda raslimali za misitu hapa Nchini ili kuondokana na uvamizi wa maeneo ya misitu.
Kauli hiyo imetolewa leo Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhandisi RAMO MAKANI alipokuwa akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo mpya ambapo amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizobarikiwa kuwa na rasilimali kubwa ya misitu lakini changamoto kubwa ni uvamizi wa maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya hifadhi za misitu.
Amesema kuwa maeneo hayo yamekuwa yakitumika kwa shughuli za kibanaadamu badala ya shughuli iliyokusudiwa hivyo anaamini kamati hiyo itaongeza juhudi za kuisaidia Serikali katika kulinda rasilimali za misitu ya Taifa ili iweze kuchangia kwenye pato la taifa .
Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo Profesa REUBEN MWAMAKIMBULAH amesema kuna tatizo la migogoro na usimamizi wa misitu ndani ya misitu ambapo kumekuwa na idadi kubwa ya wahalifu wanaojificha katika hifadhi za misitu
MSAFIRI CHAGAMA NA GLADNESS MKAMBA ni baadhi ya wajumbe wa Kamati wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema kuwa wamejipanga katika kulinda rasilimali ya misitu nchini kwa kuhakikisha wanatoa elimu kwa jamii ili ifahamu umuhimu wa kulinda misitu.