- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SERIKALI YAUNDA KAMATI KUCHUNGUZA UBADHILIFU WA FEDHA ZA UMMA
DODOMA: OFISI ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) imesema itatuma timu maalum wiki ijayo kwenda kufanya uchunguzi wa haraka kufuatia kuwepo na harufu ya ubadhirifu wa fedha za umma katika Halmashauri ya wilaya ya Hanang mkoani Manyara.
Naibu Waziri wa wizara hiyo SELEMAN JAFO ametoa Kauli hiyo leo bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti maalum ROSE KAMILI.
Katika swali lake mbunge huyo ametaka kujua ni kigezo gani kimetumika kuwaacha watumishi waliofanya ubadhirifu kwenye halmashauri hiyo kuendelea kuwa kazini.
Akijibu swali hilo JAFO amesema wizi ni wizi hakuna wizi mdogo wala mkubwa na kwamba Halmashauri hiyo inaonekana kuna madudu makubwa.
Kwa upande wake waziri wa wizara hiyo GEORGE SIMBACHAWENE akitoa majibu ya nyongeza katika suala hilo amesema ubadhirifu mwingi unaofanyika kwenye halmashauri ni kubadilisha matumizi ya fedha na hivyo kusisitiza kuwa kuanzia sasa utaratibu huo umebadilishwa.