- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SERIKALI YATOA ONYO KWA WATUMISHI WANAOHUSIKA NA UJENZI WA VITUO VYA AFYA.
DODOMA: Serikali imesema kuwa haitamfumbia macho kiongozi au mtumishi yeyote ambaye atatumia vibaya fedha zilizotolewa kwajili ya ujenzi na ukarababti wa vituo vya afya 172 nchini.
Kauli hiyo imetolewa na katibu mkuu ofisi ya waziri mkuu Maimuna Tarishi alipokuwa akifunguamkutano wa viongozi na watendaji wa ujenzi na ukarabati wa vituo vya afya nchini uliofanyika leo mjini Dodoma .
Aidha amesema kuwa katika zoezi hilo hatarajii kuona mkurugenzi yeyote anakwenda kinyume na ramani za ujenzi zirizotolewa na serikali kwa madai kuwa fedha hizo hazitoshi.
Katika hatua nyingine Tarishi amesema kuwa serikali ipo katika mkakati wa ukarabati na ujenzi wa vituo vya afya nchini kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma na kupunguza vifo vya mam na mtoto ambavyo hadi sasa vimefika vifo 556 kwa vizazi hai 100,000.
Pamoja na hayo Amesema, kwamwaka huu watakarabati jumla ya vituo vya afya 172 ambapo ubarozi wa Canada umetoa kiasi cha Dola za marekani milioni 22 zinazotumika kukarabati vituo 44, Benki ya dunia imetoa Dola za marekani milioni 66 kwa ajili ya kukarabati vituo 103.
Pia vituo vya afya 25 vitafanyiwa ukarabati kupitia frdha za benki ya Dunia na mfuko wa afya wa pamoja kwa fedha zilizo vuka mwaka kwa mwaka fedha 2016/17 ambapo fedha za kitanzania bilioni 12.5 zitatumika.
Kwa upande wake katibu mkuu Ofisi ya Rais Tamisemi Mhandisi Mussa Iyombe, amesema kuwa sekta ya afya bado inachangamoto nyingi ikiwemo ile ya ukosefu wa majengo.
Hata hivyo amesema kuwa ujenzi pamoja na ukarabati huo unatarajiwa kukamlika ifikapo Disemba 30 mwaka huu na tayari serikali imeshapeleka kiasi cha shilingi milioni 500 kwa kila kituo kwa vituo vyote 172.