- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SERIKALI YATOA KIFUTA JASHO KWA WANYAMAPORI
DODOMA: WIZARA ya Maliasili na Utalii imesema,hailipi fidia kwa madhara yanayosababishwa na wanyama pori hatari au waharibifu na badala yake inatoa kifuta jasho au kifuta machozi.
Akijibu swali Bungeni LEO Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhandisi Ramo Makani amesema ,Serikali inafanya hivyo kwa mujibu wa kifungu cha 68 (I) cha Sheria ya kuhifadhi Wanyamapori Namba 5 ya mwaka 2009.
Aidha Makani amesema kifungu cha 3 cha kanuni za malipo ya kifuta jasho na kifuta machozi za mwaka 2001,kinaashiria masharti ya viwango vya malipo ya kifuta jasho na kifuta machozi.
Wizara yangu imepokea madai ya wananchi 5 waliouawa,4 waliojeruhiwa na 31 waliharibiwa mazao yao,madai hayo yamefanyiwa kazi kwa mujibu wa kanuni na yatalipwa mara fedha zitakapopatikana
Mhandisi Makani alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Mbulu Mjini Zakaria Issaya(CCM) ambaye amehoji Serikali kwamba lini itawalipa fidia wananchi wapatao sita wilayani Mbulu walioshambuliwa na kuuawa na Wanyamapori Kati ya Juni na Desemba mwaka jana.
Mbunge huyo pia ametaka kujua ni lini Serikali itawalipa fidia ndugu wa hao watu sita waliouwawa na wanyama wakati tofauti katika Halmashauri ya Mji wa Mbulu na lini Serikali kupitia Tanapa italipa fidia kwa wale wote walioharibiwa mazao shambani mwaka 2014-2015’’aliuliza Issaya.