Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 1:25 pm

NEWS: SERIKALI: YATEMA CHECHE HAITOSITA KUWACHUKULIA HATUA WAZAZI WATAKAOSHINDWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO KWA WATOTO WAO

DODOMA: IKIWA leo ni siku ya familia Duniani Serikali imesema kuwa haitosita kuwachukulia hatua kali za kisheria wazazi wote wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao ya malezi kwa watoto sambamba na kuzitaka sekta binafsi na umma kuzingatia haki ya mama kunyonyesha kwa kipindi cha miezi sita ili kujenga msingi imara wa malezi na makuzi kwa mtoto mchanga.

Kauli hiyo imetolewa leo Mjini Dodomaa na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,jinsia,wazee na watoto mh.UMMY MWALIMU wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo ameeleza kuwa sheria ya mtoto inasema jukumu la kwanza la malezi ni la mzazi mwenyewe.

Aidha MWALIMU ameongeza kuwa ili kuchochea malezi bora serikali imefanyia marekebisho ya kanuni ya sheria za kazi na mahusiano kazini na kuwa sasa mama aliyejifungua ana haki ya kunyonyesha kwa muda wa masaa mawili kwa kipindi cha miezi sita mara baada ya kutoka likizo ya uzazi.

Hata hivyo kwa kutambua umuhimu wa siku Mwenyekiti wa Mtaa wa Osterbay Kata ya Kiwanja cha ndege Manispaa ya Dodoma bw.SAID SUFIAN Amekiri kuwepo kwa tatizo la malezi bora katika mtaa wake na kupelekea watoto kujiingiza katika vitendo vya uhalifu.

Kumekuwa na matukio mengi kwa watoto kujiingiza katika vitendo viovu ikiwemo vya madawa ya kulevya.