- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SERIKALI YATANGAZA NEEMA YA MAFUTA KWA WATANZANIA.
DODOMA: Serikali imesema hakuna uhaba wa nishati ya mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa kwa ajili ya matumizi mbalimbali, kwani akiba iliyopo inatosheleza kwa zaidi ya siku thelathini zijazo.
Hayo yameelezwa Jijini Dodoma na waziri wa nishati Dkt. MEDARD KALEMANI wakati akitangaza uteuzi wa wajumbe wa bodi ya ushauri ya wakala wa uagizaji wa mafuta kwa pamoja PBPA.
Dkt. Kalemani amesema akiba iliyopo katika mafuta ya petroli ni lita za ujazo milioni 39 huku mahitaji ya kwa siku yakiwa ni lita milioni 3.2 na dizeli akiba iliyopo ni lita milioni 151 na mahitaji yake kwa siku yakiwa ni lita milioni 5.2.
Kwa upande wa mafuta ya ndege waziri Kalemani amesema nchi ina akiba ya lita milioni 16.8 wakati mahitaji kwa siku ni lita laki 5.6.
Amesema matumizi ya mafuta ya taa kwani mahitaji kwa siku ni lita laki 1.4 huku akiba ikiwa ni lita milioni 5.3 hali inayoashiria ongezeko la wananchi wanaotumia umeme kutokana na uwepo wa wakala wa usambazaji wa umeme vijijini.
Mbali na hayoWaziri amewateuwa Wajumbe wanne na watahudumu kwa miaka mitatu katika chombo hicho cha ushauri chini ya mwenyekiti Dkt.Lutengano Mwakahesya aliyeteuliwa na Rais Dkt. Magufuli Novemba 22 mwaka 2018 baada ya kufariki kwa aliyekuwa mwenyekiti wa PBPA Steven Ndaki.
Waziri Kamteuwa Dk. Henry Chalu mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam(UDSM) , Salum Nassor Mnuna Afisa TEHAMA Mkuu, Wizara ya Nishati, Senzo Frederick Gwanchele kuwa Meneja, Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA)na Karolius Constantine Misungwi Mkurugenzi Msaidizi (Utawala), Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT),ββ