- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SERIKALI YATAKA WALIOSHINDWA KUENDESHA VIWANDA KUWAPA WENGINE
DODOMA: SERIKALI imewataka wawekezaji wote ambao wameshindwa kuviendesha viwanda ambavyo vilibinafsishwa kuvirejesha mara moja kwa kuwapa wengine wenye uwezo wa kuviendesha ili kutoa ajira.
Kauli hiyo ilitolewa ujana Mjini Dodoma na Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji,CHARLES MWIJAGE wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
Waziri MWIJAGE alisema kuwa Serikali kupitia kamati maalum ambapo msimamizi wake ni yeye mwenyewe na mwenyekiti wake ni Msajili wa hazina,wajumbe ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Wizara za kisekta pamoja na mwanasheria mkuu wa Serikali wao ndio wataaangalia nani anayefaa kupewa viwanda hivyo ambavyo havifanyi kazi.
Hata hivyo Waziri Mwijage alisema kuwa tayari serikali imefufua viwanda 11, ambapo vilivyofungwa ni56,vilivyobinafsishwa ni 10 huku viwanda 28 vikiwa vinasuasua na vinavyo Fanya kazi hivi sasa in 62 tu.
Aidha alisema wana mkakati wa viwanda vya Pamba,korosho pamoja na Nyama kuanza kazi mara moja.
Pia amemuagiza msajili wa hazina kuvikamata na kuvifungia baadhi ya viwanda ikiwemo Mkata kilichopo Morogoro na kiwanda cha korosho lindi.
Halikadhalika Waziri Mwijage amewataka watanzania kununua bidhaa za Tanzania ili kuinua viwanda na kukuza uchumi wa nchi.