Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 10:53 am

NEWS: SERIKALI YAPAA YAZINDUA KITABU ILI KUGUNDUA MAGONJWA SUGU

DODOMA: Serikali kupitia wizara ya afya nchini imezindua kitabu maalumu, lengo ikiwa ni kugundua baadhi ya magonjwa kama kifua kikuu pamoja na kisukari kwa mtu ambaye hana uwezo wakujieleza na anasumbuliwa na aina gani ya ugonjwa.

Uzinduzi huo umefanyika mkoani Dodoma ukihudhuriwa na mgeni rasmi naibu waziri wa afya Mhe. Dkt Hamisi Kigwangala.

Akieleza dhumuni la uanzishwaji wa kitabu hicho mbele ya mgeni rasmi Dokta Otilia Gowele ambaye ni kaimu katibu mkuu idara kuu ya afya amesema sasa hivi kuna changamoto ya baadhi ya wagonjwa kushindwa kutoa maeelezo yanayojitosheleza kwa wahuduma za afya katika zahanati mbalimbali hivyo kupitia kitabu hicho itasaidia wagonjwa hao kutoa taarifa kwa hiyari.

Dokta Otilia amesema zoezi hilo linahitaji usimamizi wa kina na wenye mpangilio katika kuhakikisha malengo ya uanzishwaji wa kitabu hicho yanatimia kwa kufanya hivyo itasaidia kuibua wagonjwa wengi ambao bado hawajatambua kama wameambukizwa ugonjwa wa kifua kikuu.

Ameongeza kuwa mbinu hiyo itasaidia kutokomeza magonjwa sugu ifikapo mwaka 2035 huku akisema katika mkoa wa Dodoma kuna madaktari watano wameambukizwa bila kujua kutokana na ugonjwa kusambaa kwa kasi.