Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 3:27 am

NEWS: SERIKALI YAMWAGA VITABU

DODOMA: SERIKALI imechapisha na kusambaza vitabu, chati na miongozo mbalimbali ya kufundishia na kujifunzia milioni 8.3 kwa ajili ya darasa la kwanza na la pili na tayari vimeshasambazwa katika shule za msingi nchini.

Naibu waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa(TAMISEMI)SELEMAN JAFO amesema hayo leo bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalum GRACE TENGEGA.

Katika swali lake mbunge huyo ametaka kujua mpango wa serikali wa kuboresha zana za kufundishia ili kwenda sambamba na ukuzaji wa ujuzi wa stadi za taalumawanazosoma.

Akijibu swali hilo JAFO amesema usambazaji wa vitabu hivyo umeboresha uwiano kwa kuzingatia Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) ya mwaka 2015.

Amesema serikali kupitia ofisi ya rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora inafanya mapitio ya majukumu ya watumishi wote wakiwemo walimu ili kuboresha maslahi ya watumishi wote kwa kuzingatia uzito wa kazi.