- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SERIKALI YAKIRI UPUNGUFU WA NYUMBA 10,297 KWA ASKARI
DODOMA: Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mwigulu Nchemba amekiri kuwa Serikali ina upungufu wa nyumba 10,297 hali ambayo inasababisha baadhi ya askari kuishi nje ya kambi.
Nchemba ametoa kauli hiyo leo bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Mchinga, Hamidu Bobali (CUF)
Bobali alietaka kujua kuhusina na Gereza la Kingulungundwa lilopo Wilayani Lindi kukabiliwa na uhaba mkubwa wa nyumba za askari na miundombinu mibovu.
‘’Je serikali ina mpango gani wa kuboresha makazi ya askari katika gereza hilo?
‘’Gereza hili lipo umbali wa km 3 kutoka barabara kuu inayotoka Dar es salaam kwenda Lindi lakini wakati wa Masika barabara hiyo haipitiki kwa gari kutokana na kujaa tope na maji’’
‘’Je Serikali haioni kuwa kukosekana kwa mawasiliano na barabara kutoka katika gereza ni jambo la hatari?’’alihoji
Akijibu swali hilo,Mwigulu amesema mahitaji ya nyumba za askari Magereza hivi sasa ni nyumba 14500 ambapo zilizopo ni 4221 hivyo kuwepo na upungufu wa nyumba 10,279 ambao unasababisha askari kuishi nje ya kambi.
Serikali inafahamu kuwa lipo tatizo la uchakavu na upungufu wa nyumba za askari wa jeshi la Magereza nchini na hali hiyo inatokana na baadhi ya nyumba kujengwa kabla ya uhuru.
Amesema kwa sasa serikali ina mpango wa kuwajengea askari Magereza nyumba 9500.
‘’Mara baada ya mpango huo kukamilika tunategemea kumaliza kero ya makazi ya askari nchini likiwemo gereza Kingulungundwa’’amesema
Mwigulu amesema kwa sasa Jeshi la Magereza litajenga nyumba 320 za Maafisa na askari Ukonga fedha ambayo imetolewa na Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kiasi cha Shilingi 10,000,000,000.00.
‘’Ni kweli Barabara inayotoka Barabara kuu ya Dar es salaam- Lindi kuelekea gereza la Kingulungundwa imekuwa haipitiki kwa gari wakati wa masika kimsingi barabara hiyo ipo chini ya Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Vijijini na ndiyo yenye jukumu la kuifanyia matengenezo.
Amesema Jeshi la Magereza limekwishafanyiwa mawasiliano na Mkurugenzi wa Wilaya ya Lindi Vijijini ili barabara hiyo iweze kutengenezwa kuepusha adha inayojitokeza wakati wa masika