- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SERIKALI YAKILI UBAMBIKIWAJI WA BILI ZA MAJI KWA WANANCHI
DODOMA: WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji,Isack Kamwelwe amekiri kuwa kumekuwa na tatizo la ubambikiwaji wa bili za Maji kwa Wananchi unaofanywa na Mamlaka mbalimbali za maji nchini.
Akijibu swali jana bungeni la nyongeza la Mbunge wa Songea Mjini,Leonidas Gama (CCM) ambaye alidai kuwa kumekuwa na tatizo la ubambikizwaji wa bili za maji hivyo ni lini Seriklali itasimamia jambo hilo kwani limekuwa likiwapa usumbufu mkubwa wananchi.
Kamwele alikiri kuwepo kwa tatizo hilo huku akidai tayari wameanza kulifanyia kazi kwani hata Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk John Magufuli aliagiza suala hilo lishughulikiwe.
Katika swali la msingi Gama alihoji kuhusina na Mji wa Songea kuwa una matatizo makubwa na Halmashauri hiyo inategemea visima virefu na vifupi na maji mtiririko.
‘’Je Serikali haioni umuhimu wa kulighulikia suala hilo na Je Serikali haioni kuwa ikiondoa tatizo hilo itakuwa imemaliza kero kubwa kwa Wananchi zaidi ya 30,000 ambapo kila kituo kitakuwa kikihudumia watu 250’’aliuliza Gama.
Akijibu Kamwelwe alisema Mji wa Songea una jumla ya watu wapatao 230,000 ambapo katika maeneo ya Mjini kunakadiriwa kuwa na jumla ya Wananchi 194,000 na pembezoni wakazi wapatao 36,000.
Alisema maeneo ya pembezoni mwa Mji huo kuna vituo vya kuchotea maji 187 vilivyogawanjika katika makundi mawili ambapo kundi la kwanza ni visima vifupi 89 na kundi la pili ni vikundi vya kuchotea maji kutoka katika mradi wa maji mtiririko.
‘’Serikali ilikwishaona umuhimu wa kumaliza tatizo la maji katika manispaa ya Songea na kwa mwaka wa fedha 2016-2017 kiasi cha Shilingi milioni 314 kwa ajili ya ukarabati wa visima vifupi 89 ambavyo ufanisi wake umepungua’’alisema