Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 5:25 pm

NEWS: SERIKALI YAJIPANGA KUMALIZA TATIZO LA MADAWA YA KULEVYA

DODOMA: SERIKALI imesema kupitia kamishna wa dawa za kulevya nchini wametengeneza mpango mkakati maalum wa kuhakikisha tatizo la dawa za kulevya linaondoka nchini.

Hayo yameelezwa leo bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Ajira,Vijana na Walemavu JENISTA MHAGAMA wakati akijibu swali la mbunge wa Konde KHATIB SAID HAJI na mbunge wa Viti maalum RITHA KABATI.

Katika swali lake HAJI ametaka kujua serikali itachukua jitihada gani za makusudi za kukabiliana na uingiizaji wa dawa za kulevya Zanzibar ambako inasemekana ni lango kuu la kupitisha dawa hizo.

Kadhalika KABATI ameihoji serikali ina mpango gani wa kuvipa ruzuku vituo binafsi vya kutolea huduma ya Methodone Iringa.

Waziri MHAGAMA amesema Mpango huo mkakati utatekelezwa kwa kushirikisha Tanzania Bara na Zanzibar.