- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SERIKALI YAJIPANGA KUCHIMBA VISIMA VIJIJINI
DODOMA: NAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo amesema visima vingi hasa vilivyochimbwa na kufungiwa pampu hukauka wakati wa kiangazi katika kwenye maeneo mbalimbali nchini.
Jafo ametoa kauli hiyo leo Bungeni alipokuwa akijibu swali Mbunge wa Viti maalum(chadema), Joyce Sokombi .
Sokombi ametaka kujua ni lini serikali itahakikisha programu za maji zinapelekwa na zinatekelezwa kwa umakini katika Wilaya ya Musoma Vijijini.
“Kumekuwa na tatizo kubwa la maji katika Wilaya ya Musoma Vijijini hasa Vijiji vya Kabulabula, Bugoji, Kangetutya na Saragana, visima vilivyochimbwa na wanakijiji hao vinakauka wakati wa kiangazi,”amesema Mbunge huyo
Akijibu swali hilo, Jafo amesema kutokana na kukauka wakati wa kiangazi huathiri upatikanaji wa huduma katika maeneo husika.
Ameaja sababu kubwa ni mabadiliko ya tabia YA nchi hali iliyosababisha maji kupatikana katika kina kirefu zaidi.
Kwa kutambua hilo, Jafo amesema serikali kupitia program ya Uendelezaji wa sekta ya Maji(WSDP II), imeanza kufanya usanifu wa mradi mpya utakaotumia Ziwa Viktoria kama chanzo cha uhakika.
“Vijiji vitakavyoingizwa katika mpango huo ni Kaburabura,Bugoji na Saragana,”amesema Naibu Waziri Jafo.