- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SERIKALI YAFANYA JUHUDI KUTATUA MGOGORO WA ARDHI YA KAMPUNI YA HIGHLAND ESTATE MBARALI
DODOMA: MBUNGE wa Viti Maalum, Sophia Mwakagenda (Chadema) jana aliibana serikali na kuitaka ieleze ni lini itatatua mgogoro wa ardhi kati ya kampuni ya Highland Estate Mbarali na wananchi wanaozunguka shamba hilo kwa kuwa mwekezaji amekuwa akipora ardhi wa wananchi na kusababisha uvunjifu wa amani kwa muda mrefu sana.
Mwakagenda alitaka serikali itoe majibu hayo jana bungeni wakati akiuliza swali la msingi kwa maelezo kuwa mwekezaji huyo kwa sasa amekuwa mwiba kwa wananchi wanaozunguka shamba hilo kutokana na kukosa amani kutokana na kuwepo kwa mgogoro huo.
Akijibu swali la Msingi Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Angella Mabula,alisema shamba linalomikiliwa na kampuni hiyo awalai lilikuwa linamilikiwa na Shirika la taifa la Kilimo na Chakula kuanzia mwaka 1978.
Alisema baada ya upimaji kukamilika mwaka 1981 shamba hilo liliendelea kumilikiwa na NAFCO kwa hati Na. 327-DLR na 18 August2008 shamba hilo liliuzwa na serikali kwa kampuni ya Highland Estate Ltd.
Mabula alisema mgogoro wa shamba hilo unahusu tafsiri ya mipaka baina ya shamba hilo na vijiji vya Mwanavala,Ibumila,Songwe,
Alisema hatua za awali za kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huo zinahitaji kupata tafsiri sahihi ya mipaka wa shamba kulingana na ramani ya upimaji iliyoidhinishwa na mkurugenzi wa upimaji na ramani ya wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja na vijiji vilivyozunguka shamba hilo.
“Zoezi la kutafsiri mipaka baina ya shamba na na vijiji husika limeisha anza kufanywa na wataalam wa ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbarali pamoja na ofisi ya Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mbarali kwa kushirkiana na vijiji husika isipokuwa wanakijiji wa kijiji cha Nyelegete ambao wamesusia zoezi hilo” alieleza Mabura.
Aidha alisema juhudi za kutatua mgogoro huo bado zinaendelea kufanywa na Mkuu wa Wilaya ya Mbarali pamoja na mkurugenzi wa halmashauli ya Mbarali kwa kuwahimiza kijiji cha Nyeregete kutoa ushirikiano kwenye utatuzi wa mgogoro huo ili uweze kumalizika.