Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 4:29 pm

NEWS: SERIKALI YAAHIDI KUSIMAMIA UPOTEVU WA FEDHA ZA UMMA.

DODOMA: Serikali imeahidi kusimamia kikamilifu utekelezaji wa mpango‘programu’ wa maboresho ya usimaminzi wa fedha za umma awamu ya tano ili uweze kuleta manufaa kwa umma na kuthibiti upotevu wa mapato ya serikali.

Hayo yameelezwa na makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan wakati wa uzinduzi wampango ‘programu’ wa maboresho ya usimaminzi wa fedha za umma awamu ya tano uliofanyika mjini Dodoma .

Hata hivyo makamu Samia amewaagiza watendaji wote wa serikalikuhakikisha wanatekeleza program hiyo kwa umakini mkubwa kws kuimarisha mifumo ya usimaminzi wa fedha za umma.

Naye waziri wa fedha na mipango Dkt. Philip Mpango amesema kuwa programu ya maboresho na usimamizi wa fedha za umma , utaongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato ya serikali na kuthibiti mianya yote ya matumizi mabaya ya fedha za umma.

Baadhi ya wadau wa maendeleo kutoka maeneo mablimbali duniani ambao wanashirikiana na Tanzania wameridhishwa na hatua mbalimbali za maendeleo zilizofikiwa na serikali ikiwemokupiga vita rushwa ,uzembe kazini na kusimamia ipasavyo ukusanyaji wa mapato na kuthibiti matumizi yasiyo na tija.

Uzinduzi huo umekuja baada ya program ya nne kuishiaa mwezi juni mwaka huu

Ambapoprogramu hiyo ya miaka mitano .itahusisha mikoa yote 26 ya Tanzania Bara na Zanzibar ikiwa na lengo la kuongeza uwajibikali, uwazi, usimamizi wa bajeti katika kulinda rasilimali za nchi.