- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SERIKALI SASA KUZIBA MAPENGO YA VYETI FEKI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki alisema hayo jana jijini Dar es Salaam alipokutana na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kusikiliza changamoto zao na kuzitafutia ufumbuzi.
Alisema sasa serikali imepanga kutoa ajira maalumu kwa kila halmashauri ili kujaza nafasi za watumishi walioondolewa kazini baada ya kubainika kugushi vyeti pamoja na wengine waliokuwa na vyeti feki.
“Nikianzia na Halmashauri ya Temeke, niwahakikishie kuwa tatizo la watumishi litapungua na pia kwenye kila manispaa iliyoondokewa na wafanyakazi kwa sababu ya vyeti feki, watapewa idadi ileile ya watu ili waweze kujaza nafasi zao na hivyo, kuziba mapungufu waliyoyaacha,” alisema Waziri Kairuki. Alisema zaidi ya watumishi 133,000 wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke watapandishwa vyeo katika kipindi cha Mwaka wa Fedha wa 2017/18.
source: habarileo