- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SERIKALI MBIONI KUJENGA JENGO LA UPASUAJI ULANGA.
MOROGORO: Wananchi wa wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro wameipongeza serikali kwa kukamilisha ujenzi wa daraja la kilombero ambalo lilikuwa kero kubwa kwa muda mrefu.
Wananchi hao wametoa pongezi hizo leo kupitia kwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo alipokuwa katika ziara ya kikazi.
Wananchi hao wamesema wanaishukuru Serikali kwani walikuwa wakipata shida kubwa na adha hiyo ilisabbaisha baadhi ya wananchi wamepoteza maisha
Katika ziara yake Naibu Waziri Jafo amefanikiwa kukagua miradi ya afya pamoja na kuongea na wananchi.
Akizungumza na wananchi, Naibu Waziri Jafo amempongeza Mbunge wa Jimbo hilo Goodluck Mlinga kwa kuisaidia ukarabati wa wodi ya wazazi katika kituo cha Afya Lupilo kwa kutumia mfuko wa Jimbo.
Naibu Waziri Jafo amewaambia wananchi hao kuwa serikali ipo mbioni kujenga jengo la upasuaji katika kituo hicho ili wananchi wa eneo hilo la Lupilo wilayani Ulanga waweze kupata huduma bora za Afya ili kupunguza vifo vya akinamama na watoto.