- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SERIKALI KUTUMIA DOLA 66 ZA KIMAREKANI ZA MSAADA KUJENGA VITUO VYA AFYA.
DODOMA: Naibu waziri wa nchi ofisi ya raisTAMISEMI Selemani Jafo ametoa miezi mitatu kwa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kuhakikisha wanasimamia kikamilifu ujenzi wa vituo vya afya nchini.
Ameyasema hayo leo mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari.
‘’waheshimiwa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya wahamasishe wananchi kujitolea nguvu kazi katika maeneo yao kwani ujenzi huo utatumia ‘’force akaunti’’ ambapo katika utaratibu huo itaajiri mafundi, mhandisi wa halmashauri na wataalamu wake watasimamia.’’ Asema Jafo.
Amesema katika zoezi hilo jumla ya vituo vya afya 172 vitafanyika ukarabati.
Akifafanua Jafo amesema kupitia wizara ya maendeleo jamii, jinsia na watoto serikali imepokea fedha dola za kimarekani milioni 66 kutoka benki ya dunia ambapo vituo vya afya 103 vimekarabatiwa.
Amesema kupitia ofisi ya TAMISEMI serikali ilipata msaada kutoka ubalozi waCanada wa fedha dola za marekani milioni 66 kutoka benki ya dunia ambapo vituo vyaafya 44 vitakarabatiwa.
‘’Vituo vya afya 25 vitafanyiea ukarabati kupitia fedha za benki ya dunia na mfuko wa afya wa pamoja kwa fedha zilizovuka mwaka kwa mwaka wa fedha 2016/2017 ambapo fedha za kitanzania bilioni 12. 5 zitatumika katika ukarabati huo kuila kitu kimetengemewa shilingi milioni 500’’ amesema
Jafo amesema kila katibu tawala wa kila mkoa anapaswa kuwasilisha katika ofisi ya rais TAMISEMI taarifa za kila mwezi za maendeleo ya ukarabati wa vituo hivyo katika mkoa wake
‘’kila tarehe 5 ya mwezi unaoanza [deadline] itakuwa ni siku ya mwisho ya kupokea taarifa hizo’’ amesema Jafo.
Jafo amesema matarajio ya OR TAMISEMI kuwa vituo vyote vitakuwa vimekamilika kabla ya tarehe 30 desemba mwaka huu.