- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SERIKALI KUTOKUTOZA USHURU VYOMBO VYA USAFIRI
DODOMA: SERIKALI imesema kuwa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi kavu na Majini nchini(SUMATRA) haitoi vibali wala haitozi ushuru kwa vyombo vya usafiri majini nchini ikiwa ni pamoja na wavuvi wa Ziwa Tanganyika.
Kauli hiyo imetolewa leo,Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, injinia EDWIN NGONYANI wakati akijibu swali la msingi laMbunge wa Kigoma Mjini,ZUBEIR ZITTO,ambaye ametaka kujua kuhusina na Mamlaka ya Usimamizi wa Usafiri wa Majini na nchi kavu(SUMATRA)kutoa vibali vya usafiri kwa wavuvi wa Ziwa Tanganyika.
Akijibu swali hilo,NGONYANI amesema kuwa Moja ya majukumu ya Msingi ya SUMATRA katika vyombo vya usafiri na vya majini na nchi kavu ni kuhakikisha vyombo hivyo ni salama kabla ya kuanza kufanya shughuli za majini.
Aidha amebainisha kuwa Mamlaka hiyo inapokagua vyombo vya usafiri majini kwa mujibu wa sehemu ya 11 kanuni ya 9 ya kanuni za sheria , wenye vyombo vya usafiri ikiwa ni pamoja na vya uvuvi.
Kutokana na hali hiyo,Ngonyani amesema Serikali haikusudii kudidimiza wavuvi wala haijawarundikia tozo nyingi ambazo zitawafanya wawe maskini bali inawahakikishia mazingira salama kwa ajili ya kufanya shughuli zao za uvuvi.