Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 4:41 pm

NEWS: SERIKALI KUPELEKA MAJI YA UHAKIKA NGUDU

DODOMA: SERIKALI imetekeleza mradi wa majisafi kutoka Ziwa Victoria kwenda katika mji wa Ngudu na vijiji vilivyopo kando kando ya bomba linalopeleka maji katika Mji wa Ngudu .

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isac Kamwelwe Ametoa kauli hiyo leo mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Maswa Magharibi Mashimba Ndaki (CCM) ambaye alitaka kujua kama Serikali haioni umuhimu wa kuunganisha Mji mdogo wa Malampaka katika mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria ili kuwapatia wananchi maji ya uhakika.


"Serikali imekamilisha mradi wa maji kutika Ziwa Victoria hadi Mji wa Ngudu na vijiji vilivyo karibu na Mji huo wilayani Kwimba,mradi huu unatoa maji ya uhakika kuliko miradi ya visima vifupi ambavyo ni vya msimu ,

"Lakini Mji mdogo wa Malampaka na vijiji vingine vya karibu na Jihu,Bukigi ,Muifa,Kali,Nyababinza na Mwang'horoli ambavyo vipo karibu na Mji wa Ngudu havijaunganishwa kwenye mradi huo,

"Je,Serikali haioni umuhimu wa kuunganisha Mji mdogo wa Malampaka na vijiji vya Jihu ,Bugiki,Muhida,Lali,Nyabanziba na Mwang'horoli katika mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria ili kuwapatia wananchi hao maji ya uhakika?" amehoji Ndaki



Aijibu Mhandisi Kamwelwe alisema,mradi huo ilihusisha ulazaji wa bomba la kilomita 25 na sehemu nyingine ya bomba lilitumika bomba la zamani la mradi wa visima uliojengwa miaka ya 70.

Aidha amesema,Serikali kupitia programu ya maendeleo ya sekta ya maji ,imetekeleza miradi ya maji Malampaka,Sayusayu,Mwasayi,Niapanda na Sangamwalugesha ambapo miradi hiyo imekamilika na wananchi wanapata maji.


"Serikali pia imekamilisha usanifu na uandaaji wa makabrasha ya zabuni kwa miradi ya maji ya Mwabulimu,Mwamanenge na Badi ambayo itahudumia vijiji vya Muhida,Jihu na Badi yenyewe,ujenzi wa miradi hii itafanyika katika awamu ya pili ya programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji." Lisema Mhandisi Kamwelwe

Pia amesema,Serikali imeandaa mradi wa kutoa maji za,wa Victoria kwenda kwenye miji ya Sumve ,Malampaka na Mallya ambapo hadi sasa taratibu za kumpata mtaalam mshauri atakayefanya usanifu wa mradi huo zinaendelea ambapo jumla ya shilingi bilioni mbili zimetengwa katika mwaka wa 2017/2018 kwa ajili ya mradi huo ambapo pia utanufaisha baadhi ya vijiji vilivyopo katika Mji mdogo wa Malampaka.