- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SERIKALI KUONDOA TOZO ZA MAZAO
DODOMA: SERIKALI imesema ipo tayari kuondoa kodi na tozo mbalimbali za mazao ya kilimo,mifugo na uvuvi zisizokuwa na tija kama ilivyofanya mwaka 2016/2017.
Aidha kwa mwaka huu imeondoa jumla ya tozo 80 na kupunguza viwango vya tozo 4 katika tasnia ya mazao pekee kati ya jumla ya tozo 139 zilizopo.
Hayo yameelezwa leo bungeni mjini Dodoma na waziri wa kilimo,Mifugo na Uvuvi WILLIAM OLE NASHA wakati akijibu swali la mbunge wa Kyerwa INNOCENT BILAKWATE.
OLE NASHA amesema ni matarajio ya serikali kuwa hatua hiyo itatoa matokeo yanayotarajiwa na kuwasaidia wakulima wa zao la kahawa kuongeza kipato chao huku akiwashauri kutoanza kuhangaika kutafuta soko la kahawa nje ya nchi kiholela kwa kuwa watajiingiza katika gharama zisizo na lazima na hivyo kupunguza kipato chao.
Katika maswali yake mbunge BILAKWATE ametaka kujua serikali imefikia wapi katika kuondoa ushuru na kodi zinazomfanya mkulima asione faida ya kuendelea na zao hili na kama serikali haiko tayari kuondoa tozo na kodi je ipo tayari kuwaruhusu wakulima wauze kule ambako watapata bei nzuri.