Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 3:38 am

NEWS: SERIKALI KUMILIKI 100% ZA KIWANDA CHA KUTENGENEZA MATAIRI CHA ARUSHA

DODOMA: SERIKALI imesema mpaka sasa inamiliki asilimia 100 katika kiwanda cha kutengeneza matairi cha Arusha baada ya kununua asilimia 26 ya hisa zilizokuwa zinamilikiwa na mbia mwenza.

Hayo yameelezwa jana bungeni mjini Dodoma na waziri wa Viwanda,Biashara na uwekezaji CHARLES MWIJAGE wakati akijibu swali la mbunge wa Ubungo SAED KUBENEA.

Katika swali lake mbunge huyo ametaka kujua mpaka sasa kazi ya kufufua kiwanda hicho imefikia wapi na inatarajiwa kugharimu fedha kiasi gani.

Akijibu swali hilo MWIJAGE alisema ili uwekezaji mpya katika kiwanda uwe wenye tija,katika mwaka wa fedha wa 2016/2017 serikali imefanya utafiti wa kubainisha aina ya teknolojia itakayotumika,uwezo wa uzalishaji,upatikanaji wa malighafi,upatikanaji wa soko,athari za mradi na teknolojia itakayotumika kwa mazingira.

MWIJAGE alisema serikali inakamilisha utafiti huo kwa ajili ya kukadiria gharama zitakazohitajika na kuzitumia kujadiliana na wawekezaji mbalimbali wanaojitokeza kuwekeza katika kiwanda hicho.