Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 3:25 am

NEWS: SERIKALI KULETA MWAROBAINI WA MIGOGORO YA ARDHI

DODOMA: Waziri mkuu Kassimu Majaliwa amesema serikali imejipanga kuja na tamko ambalo litahakikisha migogoro ya ardhi na ile ya wakulima na wafugaji inaondoka kutokana na masuala mbalimbali ya yanayofanywana wafugajikwa kuhama hama kila mara na kuleta usumbufu.

Waziri mkuu ameyasema hayo wakati akijibu swali la mbunge wa Liwale Mohamed Kuchauka aliyetaka kujua tamko la serikali juu ya migogoro ya wakulima na wafugaji katika maeneo mbalimbali nchini ambapo mbunge huyo amesema kuwa wafugaji sasa wameanza kuhamisha mifugo yao kwenda katika maeneo mengine na kuanzisha migogoro mipya.

Amesema serikali sasa itachukua hatua ya kuanza kuwatambua wafugaji kwa kuandikisha katika maeneo yao na kubaini kama mifugo hiyo inatosha kuwepo katika eneo husika na haitaleta matatizo ya migogoro na kusababisha mauaji kwa wananchi.