Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 5:48 pm

NEWS: SERIKALI KUJIPANGA KUHAKIKISHA HUDUMA YA CDA ILIYOKUWA INATOLEWA KUTOLEWA NA MANISPAA YA DODOMA

DODOMA: SERIKALI imejipanga kuhakikisha huduma iliyokuwa inatolewa na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu(CDA)kabla ya kuvunjwa inapatikana chini ya Manispaa ya Dodoma na hivyo imewatoa hofu wananchi.

Aidha imesema itaweka utaratibu maalum wa kubadilisha hati ya miaka 33 iliyotolewa awali katika Manispaa ya Dodoma na kupewa hati ya miaka 99 kuanzia ilipotolewa hati husika.

Naibu waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi ANGELINA MABULA ameyasema hayo leo bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa viti maalum FELISTER BURA.

Katika swali lake mbunge huyo ametaka kujua serikali itaweka utaratibu gani wa dharura wa kuhakikisha wananchi wa Dodoma wanahudumiwa wakati taratibu nyingine zinaendelea.


Amewahakikishia wakazi wa Dodoma kuwa mbali na kuvunjwa kwa mamlaka hiyo huduma zote za ardhi zinaendelea kutolewa chini ya ofisi ya mkurugenzi wa manispaa ya Dodoma.