- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SERIKALI KUIBUA VIPAJI KWA VIJANA
DODOMA: SERIKALI imesema katika jitihada za kuleta maendeleo endelevu ya mchezo wa riadha na michezo yote kwa ujumla inakamilisha mapitio ya sera ya maendeleo ya michezo ya mwaka 1995 ili kuhakikisha inaendana na mahitaji ya sasa katika maendeleo ya michezo.
Naibu waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ANASTAZIA WAMBURA amesema hayo leo bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa Mafinga Mjini COSATO CHUMI.
Katika swali lake mbunge huyo ametaka kujua serikali imejipanga vipi kuhakikisha inafufua mchezo wa Riadha ili kutumia kutangaza utalii wa Tanzania.
WAMBURA amesema wizara yake kwa kushirikiana na ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) na wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imeendesha mashindano ya Umiseta na Umitashumta ambayo pamoja na mambo mengine yanalenga kuibua na kuendeleza vipaji vya vijana wetu katika mchezo wa Riadha.
Aidha amesema serikali kwa kushirikiana na wadau inatekeleza programu mbalimbali za kuendeleza mchezo wa Riadha nchini ikiwemo Kilimanjaro Marathon,Bagamoyo Marathon,Tulia Marathon,Heart Marathon ambayo hushirikisha wanariadha kutoka nje ya Nchi.