- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SERIKALI KUBORESHA MRADI WA ELIMU YA UALIMU
DODOMA: Serikali inatarajia kutumia kiasi cha shilingi bilioni 168 katika kutekeleza mradi wa kuboresha Elimu ya Ualimu hapa nchini.
Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Simon Msanjila wakati akifungua mkutano wa wadau wa kuwasilisha taarifa ya mahitaji ya vyuo vya ualimu vinavyotoa mafunzo ya astashahada na shahada uliofanyika mjini leo mjini hapa.
Amesema,mradi huo unatekelezwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Serikali ya Canada huku akisema mradi huo utafanyika kwa kipindi cha miaka mitano.
Amesema,mradi huo ambao umeanza tangu mwezi Machi mwaka huu ,una lengo la kuboresha ufundishaji na ujifunzaji katika vyuo vya ualimu vya serikali ili kuandaa walimu bora wa ngazi zote kuanzia shule za awali mpaka sekondari.
“Ili kufanikisha lengo hili maeneo ambayo yataguswa ni pamoja na kuboresha miundombinu ya vyuovyote 35 vya ualimu vya serikali ,upatikanaji wa vifaa vya ufundishaji na ujifunzaji,kuboresha mtaala wa elimu ya ualimu na ili mtaala utekelezeke wafukunzi wa vyuo vya ualimu watafanyiwa mafunzo ya huo mtaala mpya ili wakautekeleze kwa ufanisi”amesema Profesa Simon
Amewataka wadau hao kutumia siku mbili za mkutano huo kuyafanyia kazi watakayoyajadili ili kufanikisha malengo ya mradi huo.
Amesema,mradi huo ni katika miradi mingi na uwekezaji mkubwa ktika sekta ya elimu unaofanywa na Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maedeleo ikiwemo Serikali ya Canada ambae ni mdau mkubwa katika uwekezaji kwenye sekta ya elimu .
Vile vile alisema,katika mwaka huu wa fedha Serikali kupitia Wizara ya Elimu ,Sayansi na Teknolojia ,imejipanga kuwekeza sana kwenye miundombinu ya elimu kuanzia ngazi ya chini kabisa mpaka vyuo vikuu.
“Lakini pia Serikali na wadau wa maedeleo katika mwaka huu wa fedha, itaimarisha miundombinu ya vyuo vikuu kwa lengo la kuboresha utoaji wa elimu ngazi ya vyuo vikuu.”amesisitiza