- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SERIKALI KUBADILI MFUMO MZIMA WA ELIMU NCHINI
DODOMA: WIZARA ya Elimu,Sayansi,teknolojia na Ufundi imesema kwa sasa inafanya mabadiliko ya mfumo mzima wa elimu ili uende sambamba na sera ya Elimu na Mafunzi ya mwaka 2014.
Kauli hiyo,imetolewa leo Mjini Dodoma na Naibu waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia mhandisi STELLAH MANYANYA wakati akijibu swali la mbunge wa Urambo MAGRETH SITTA.
Katika swali lake Mbunge huyo ametaka kujua sababu ya serikali kutounda chombo kinachojitegemea cha ukaguzi wa elimu.
Akijibu swali hilo mhandisi MANYANYA amesema idara ya Ukaguzi wa Shule iliundwa kwa mujibu wa sheria ya Elimu Sura ya 353 ya sheria za Nchi ambao ina jukumu la kufuatilia ubora wa elimu ya msingi, sekondari na Vyuo vya ualimu kwa kuzingatia viwango vya utoaji wa elimu vilivyowekwa.
Amesema kwa kuwa Idara hiyo ilianzishwa kwa mujibu wa sheria ya Elimu kwa sasa Wizara inafanya mabadiliko hayo.
Hata hivyo amesema suala la Ukaguzi wa shule kuwa chombo kinachojitegemea litaangaliwa kwa mapana katika hatua za kufanya mabadiliko ya sheria hiyo pamoja na sheria nyingine ambazo zitaweza kuongeza ufanisi katika ukaguzi wa shule.