Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 9:17 pm

NEWS : SERIKALI IPO TAYARI KUMTIBU LISSU POPOTE DUNIANI

Serikali yasema ipo tayari kugharamia matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Antiphas Lissu popote Duniani, pindi itakapopata maombi kutoka kwa familia pamoja na taarifa kutoka kwa madaktari kuhusu mahitaji ya matibabu zaidi ya mgonjwa#Waziri Ummy Mwalimu


Aidha, Serikali imeshangazwa na taarifa za upotoshaji na dhana ya kuchangishana kwa ajili ya matibabu ya Mhe. Lissu, akiwa Mtanzania na Mbunge, Serikali inayo wajibu wa kugharamia matibabu yake hadi apone ili aweze kuendelea na kazi ya kuwatumikia watanzania na wana Singida Mashariki#Waziri Ummy Mwalimu