Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 8:07 pm

NEWS: SERIKALI INAMPANGO GANI KUFUATILIA MATUMIZI MABAYA YA MASHINE YA KUSAGA NA KUKOBOA ?

DODOMA: MBUNGE wa Viti Maalum Rhoda Kunchela (Chadema) ameitaka serikali kufuatilia na kutoa taarifa juu ya matumizi mabaya ya mashine ya kukoboa na kusaga ambayo ilinunuliwa kwa zaidi y ash. Milioni 100 kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Mpanda.

Kunchela ametoa kauli hiyol eo bungeni wakati akiuliza swali la nyongeza ambapo aliitaka Serikali itoe kauli juu ya matumizi mabaya juu ya mashine hiyo ambayo kicha ya kununuliwa kwa bei kubwa lakini kwa sasa haijulikani ilipo na jengo lililojengwa kwa ajili ya kuweka mashine hiyo limekuwa gofu.



“Kwa kuwa nchi bado inakabiliwa na upungufu wa Viwanda na kunasera ya kuifanya nchi kuwa ya viwanda, Serikali inatoa kauli gani juu ya ununuzi wa Mashine ya kukoboa na kusaga ambayo ilinunuliwa na halmashauri ya Mapanda kwa zaidi y ash.milioni 100.?"

“Je kutokana na hali hiyo serikali inatoa kauli gani ili kuhakikisha mashine hiyo inarejeshwa kwa ajili ya kuwasaidia wananchi waliokusudiwa na je, Waziri wa Viwanda yupo tayari kufika katika halmashauri ya Mpanda ili kuweza kubaini ni walipi ilipo mashine hiyo ili iweze kutumiwa kwa matumizi yaliyokusudiwa” amehoji Kuchela.



Akijibu swali hilo Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage amesema kutokana na kuwepo kwa malalamiko hayo atafanya ziara katika mikoa ya Rukwa na Katavi pamoja na kufuatilia Mashine hiyo ili iweze kujulikana ni wapi ilipo na inafanya nini.