- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SERIKALI HAITA WAFUMBIA MACHO WANAOFUJA MALI ZA UMMA
DODOMA: SERIKALI imesema kamwe haiwezi kuwafumbia macho watu ambao wamekuwa wakijihusisha na ubadhilifu wa mali ya Umma, wale watakao bainika watachukuliwa hatua kali za kisheria .
Kauli hiyo imetolewa leo bungeni na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI,Selemani Jafo alipokuwa akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Viti Maalum, Rhoda Kunchela (Chadema).
Katika swali la nyongeza la mbunge huyo alitaka kujua serikali inachukua hatua gani kwa baadhi ya watendaji wa serikali pamoja na mzabuni ambaye alipewa tenda ya kununua gari la kuzolea taka na kutengwa kwa sh. Milioni 200 lakini gari hilo halikununuliwa hadi leo.
Pia alitaka kujua ni utaratibu gani wa serikali ambao umekuwakuwalazimisha wafanya biashara kufunga maduka yao kuanzia saa moja hadi saa nne kwa ajili ya kufanya usafi kwa siku ya juma mosi ya kila mwisho wa mwezi.
“Mkoa wa Mpanda kupitia halmashauri yake ilitenga kiasi cha sh. Milioni 200 kwa ajili ya ununuzi wa gari ya kuzolea taka lakini kutokana na kuwepo kwa watumishi wa serikali ambao siyo waaminifu wameshirikiana na mzabuni mr Kisila kwa kula hela hizo
“Pia serikali imekuwa ikiwalazimisha wafanyabiashara kufunga maduka yao kwa ajili ya kufanya usafi wa kila jumamosi ya mwisho wa mwezi, je kwa kufanya hivyo serikali haioni kama inawafanya wafanyabiashara hao kukosa kipato”alihoji Kunchela.
Awali katika swali la msingi la mbunge huyo alitaka kujua serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha Manispaa zinakuwa safi.
“Pamoja na lengo la serikali kuhakikisha Manispaa zinakuwa safi na kuzuia magonjwa ya mlipuko,Manispaa ina changamoto ya ukosefu wa vifaa kama magari ya taka.
“Je,Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha Manispaa zinakuwa safi”alihoji Kunchela.
Akijibu maswali hayo Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –TAMISEMI Selemani Jafo, amesema kuwa serikali kamwe haitafumbia macho mtu yoyote ambaye atabainika kufuja mali ya Umma.
Kuhusu suala la kufungwa kwa maduka kwa ajili ya kufanya usafi Jafo alisema suala hilo tayari Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Alisha litoela ufafanuzi wa kufanyika katika mamna inavyoweza kufanyika bila kuathiri mfumo wa uzalishaji.
Aidha amesema kwa sasa Manispaa ya Mpanda ina malori 2 kati ya 4 yanayohitajika kwa ajili ya kuzolea taka ngumu kutokana na changamoto hiyo wilaya ya Mpanda imejiwekea utaratibu na mikakati mbalimbali ikiwa ni pamoja na kubinafsisha shughuli za uzoaji wa taka.