- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SEREKALI YAZIPINGA TAKWIMU ZA BENKI YA DUNIA, UKUWAJI WA UCHUMI
Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Takwimu nchini Tanzania (NBS), Albina Chuwa, amesema kuwa Tanzania inaweza kutathmini takwimu za ukuaji wa uchumi wake wa mwaka 2018 baada ya Benki ya dunia kutoa takwimu zilizoonyesha kiwango cha chini cha ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo. (Reuters linaripoti.)
Bi Chuwa, ametetea njia zake na namna alivyofikia kiwango hicho,
"Tumekwenda kote nchini kukusanya data halisi , sio sawa na mtu ambaye anakaa Washington na kutengeneza sampuli za pato la ndani la nchi (GDP) kwa niaba yako,"alisema Bi Albina kulingana na Reuters
"Kwa madhumuni ya mipango ya taifa, tutaendelea kutumia data rasmi za asilimia 7.0."
Waziri wa fedha wa Tanzania aliliambia bunge mwezi uliopita kuwa kiwango cha ukuaji wa uchumi kilikuwa ni 7% mwaka jana.
Benki ya dunia ambayo ilitoa hesabu zake kwa misingi ya data za taifa , matarajio ya mwaka 2019 ya ukuaji wa kiwango cha 5.4% - pia ilitoa kiwango cha chini cha ukuaji chini ya kile kilichokuwa kimekadiriwa na na serikali cha 7.1%.
Lakini maafisa nchini humo watakutana na wawakilishi wa Benki ya Dunia mwezi Agosti kuchunguza vigezo vilivyotumiwa na benki hiyo. "Kwa hiyo tunaweza kupata matokeo mengine na tathmini ya takwimu ya pato jumla la ndani la nchi -GDP ," alisema.
Kwa mujibu wa Benki ya Dunia uchumi wa taifa la Tanzania ulikua kwa asilimia 5.2 mwaka 2018 kulingana na benki ya dunia iliosema katika katika ripoti yake kuu mwaka huu.
Ukuaji wa mwaka uliopita uliathiriwa na kushuka kwa viwango vya uwezekazji, mauzo katika mataifa ya kigeni na ukopeshaji katika sekta ya kibinfasi, ripoti hiyo imesema.
Kulinga na Reuters, data inayohusiana na matumizi, uwekezaji na biashara inonyesha kwamba ukuaji huo ulipungua mwaka 2018.
Lakini hatua ya serikali kuingilia sekta ya uchimbaji wa madini pamoja na ile ya kilimo imesababisha kupungua kwa uwekezaji katika sekta hizo katika taifa hilo linalotajwa kuwa la tatu kwa ukubwa kiuchumi Afrika mashariki, ilisema ripoti hiyo iliochapishwa na Ruters.
Kulingana na chombo hicho cha habari uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja umepungua maradufu tangu 2013, huku ukuaji wa mikopo katika sekta ya kibinafsi ukipungua na kufikia chini ya silimia 4 mwaka 2018, ikiwa ni kiwango cha chini cha wastani kati ya 2013-16.
Ripoti hiyo ya benki ya dunia inajiri kufuatia ripoti ambayo haikuchapishwa ya hazina ya shirika la fedha duniani IMF mnamo mwezi Aprili ambayo pia ilihoji jinsi rais Magufuli anavyoendesha uchumi wa taifa.
Uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja umepungua maradufu tangu 2013, huku ukuaji wa mikopo katika sekta ya kibinafsi ukipungua na kufikia chini ya silimia 4 mwaka 2018, ikiwa ni kiwango cha chini cha wastani kati ya 2013-16.
Ripoti hiyo ya benki ya dunia inajiri kufuatia ripoti ambayo haikuchapishwa ya hazina ya shirika la fedha duniani IMF mnamo mwezi Aprili ambayo pia ilihoji jinsi rais Magufuli anavyoendesha uchumi wa taifa hilo.
Katika ripoti yake, benki ya dunia WB imesema kuwa ukuaji wa kiwango cha uwekezaji ulishuka kwa sababu ya serikali kushindwa kuafikia malengo yake ya matumizi katika miradi ya maendeleo.
Ripoti hiyo inasema kwamba uchumi huo unaweza kunawiri kwa asilimia 6 kufikia 2021 iwapo kutakuwa na uimarikaji wa wa sekta ya biashara, uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja mbali na uwekezaji mwengine wa kibinafsi, ilisema benki hiyo.
Viashiria vingine vya kiuchumi pia vimeonyesha kupungua kwa kasi ya ukuaji wa uchumi.