- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SEREKALI YAWATAKA WAAJIRI WA NJEE KURITHISHA UJUZI KWA WAZAWA
"Nawapongeza TATA kwa mpango huu wa kuwajengea ujuzi Wafanyakazi wazawa,Waajiri wengine waige mfano huu wa kuja na program zenye nia ya kurithisha ujuzi kwa wafanyakazi ili kupunguza utegemezi wa wafanyakazi kutoka nje ya nchi.
Wale waajiri wenye wafanyakazi wageni na hawatekelezi mpango wa urithishaji wa Ujuzi kwa mujibu wa sheria,hatua stahiki zitachukuliwa dhidi yao kwa kukiuka utaratibu wa sheria"Alisema Mavunde.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa TATA, Rajiv Bhushan ameeleza bayana kwamba Kampuni yake imejipanga kuwawezesha Vijana wa kitanzania kwa kutekeleza program mbalimbali za mafunzo ya Ufundi na kuonesha utayari wa kushirikiana na serikali kutatua changamoto ya ukosefu wa ujuzi stahiki.
Akishukuru kwa niaba ya wanufaika wa Program hiyo Ndg Osmund Kapinga amepongeza mafunzo yanayoendeshwa na Kampuni ya TATA nchini India ambayo yanawafanya kupata ujuzi wa ziada tofauti na ufundi hali ambayo imepelekea kupata nafasi za utawala ambapo amejitolea mfano yeye mwenyewe kwa kuteuliwa kuwa Meneja wa Tawi la TATA Arusha.