Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 8:42 pm

NEWS: SEREKALI YATUMIA TRILIONI 2 KUBORESHA MAJIJI

Serikali imetumia zaidi ya Sh trilioni 2 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya kimkakati katika majiji sita nchini.

Kauli hiyo imetolewa leo Septemba 18, 2019 na Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Selemani Jaffo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo inayotelezwa na Halmashauri ya Jiji la Tanga.

Amesema kuwa miradi hiyo ina lengo la kuleta taswira mpya za kimaendeleo ikiwemo muonekano tofauti katika majiji hayo .

“Tumejenga barabara kwa kiwango cha lami na kuweka taa za barabarani, ujenzi wa madampo ya kisasa pamoja na maeneo ya kisasa ya biashara hiyo ni baadhi ya miradi ambayo inaendelea katika majiji hayo”amesema Jaffo.

Hata hivyo amewataka wakuu wa mikoa walioko katika majiji hayo kuhakikisha wanasimamia kwa ukaribu miradi hiyo iweze kuwa ni yenye viwango vyenye ubora na inayozingatia thamani halisi ya fedha.