Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 12:27 am

NEWS: SEREKALI YATOA UFAFANUZI KUFUTWA HOSPITALI YA CCBRT

Serekali imesema kuwa haina mpango wa kufuta shughuki zinazoendeshwa na Taasisi ya Hospitali ya CCBRT na PSI na badala yake kinachofanyika kwasasa ni kuhuisha usajili wa taasisi hizo kulingana na mabadiliko ya Sheria za NGO's kwasasa.

Ufafanuzi huo umetolewa leo Agosti 23, 2019 na Naibu Waziri Wizara ya Afya, Jinsia, Watoto na Wazee Dkt Faustine Ndugulile mara baada ya kusambaa kwa taarifa na mijadala inayoendelea kwenye mitandao mbalimbali ya ya kijamii kuhusu kufutwa kwa taasisi hizo.

"Ukweli ni kwamba Serikali haijasitisha shughuli za taasisi hizi. Kinachoendelea ni kuhuisha usajili wa taasisi mbalimbali ili kuendana na mabadiliko ya sheria za BRELA, RITA, SOCITIES na NGOs." amesema Dkt Ndugulile kupitia ukurasa wake wa twitter

Ndugulile amesema kuwa awali CCBRT na PSI zilisajiliwa na RITA, usimamizi wao kwa sasa utakuwa chini ya sheria ya NGOs inayosimamiwa na Wizara ya Afya. Shughuli za taasisi zinaendelea kama kawaida.

Aidha Ndugulile amewataka Watanzania kuwa na tabia ya Kuhoji kwanza ili kupata ufafanuzi kabla ya kusambaza taarifa zisizo na ukweli.
"Niwaombe watanzania kujenga utamaduni wa kupata ufafanuzi badala ya kusambaza taarifa za upotoshaji"