- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SEREKALI YATOA SABABU YA KUKATIKA KATIKA KWA UMEME
Tanga: Serekali kupitia Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amesema sababu kubwa za kukatikakatika kwa umeme nchini Tanzania kuwa hali hiyo inatokana na matengenezo makubwa yanayofanyika katika kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Ubungo Jijini Dar es Salaam.
Bi Mgalu amesema matengenezo hayo yanatarajiwa kuhitimishwa mwezi Mei 2019 ambapo tatizo la kukatika umeme litakuwa limepungua kwa kiasi kikubwa.
Kauli ya Naibu Waziri hiyo ameitoa leo Ijumaa Machi 29, 2019 wakati akizungumza na viongozi wa Wilaya ya Muheza jijini Dar es Salaam waliomlalamikia kuwa kuna changamoto ya kukatika umeme mara kwa mara.
Amesema matengenezo hayo ni makubwa ambayo Serikali imeamua kuyafanya ili kuondoa changamoto ya kukatika umeme mara kwa mara katika mikoa mbalimbali nchini.
Hata hivyo, Naibu Waziri huyo amewaagiza mameneja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) wa mikoa na wilaya kujenga mazoea ya kutoa taarifa kwa viongozi wa Serikali wa ngazi za wilaya na mikoa kuhusu sababu za kukatika umeme ili wawe wakitambua.
Kwa mkoa wa Tanga, Naibu Waziri huyo amesema umeme unakatika kutokana na wimbi la uchomaji moto misitu na mashamba ambao kwa muda wa siku tatu jumla ya nguzo 30 zilikuwa zimechomwa katika wilaya za Muheza, Korogwe na Handeni.
Amesema Wizara ya Nishati ipo katika mkakati wa kuongeza njia ya kusafirishia umeme unaotumika mkoa wa Tanga kutoka msongo mkubwa wa Kilovoti 132 za sasa hadi kufikia kilovoti 400.
Kwasasa Naibu Waziri Mgalu yupo mkoani Tanga kukagua maendeleo ya uunganishaji wa umeme vijijini kupitia Mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini (Rea) awamu ya tatu sehemu ya kwanza ambayo ina