Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 3:42 am

NEWS: SEREKALI YATOA MAAGIZO KWA BODI YA MIKOPO

Dar es Salaam. Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania imeiagiza Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kukutana mara moja na serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Daruso) kusikiliza malalamiko yao na kuyapatia ufumbuzi.

Leo Serekali ya Wanafunzi ya Chuo hicho ilitoa tamko la kuitaka bodi hiyo kutoa Mikopo kwa wanafunzi wake wanaostahiki kwa kuwapo saa 72 na iwapo hawatafanya hivyo chuo hicho kitaandamana mpaka HESLB.

Agizo hilo la limetolewa leo Jumatatu Desemba 16, 2019 na Naibu waziri wa elimu, sayansi na teknolojia hiyo, Willium Ole Nasha alipozungumza na gazeti la Mwananchi ikiwa ni saa chache kupita tangu Daruso kutoa saa 72 kwa HESLB kutoa mikopo kwa wanafunzi waliokosa, vinginevyo watakutana nje ya ofisi za bodi hiyo zilizopo Mwenge Dar es Salaam Alhamisi ya Desemba 19, 2019.

Waziri wa Habari na Mawasiliano wa Daruso, Judith Mariki alisema wamefikia uamuzi huo baada ya changamoto ya kukosekana kwa mikopo kwa wanafunzi wengi wa mwaka wa kwanza tangu chuo kifunguliwe huku baadhi ya wanafunzi wanaoendelea wakikatwa fedha zao.

“Tumesikia malalamiko yao na tayari tumeagiza uongozi wa bodi ya mikopo kwenda kuwaeleza kipi kilichosababisha tatizo hilo na hakika wataeleweshwa na wataelewa,” amesema Ole Nasha

Amesema Serikali imetoa Sh125 bilioni katika awamu ya kwanza kwa wanufaika wote lakini katika suala hilo la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuna wanafunzi wamebadili kozi na wengine kukataa rufaa, kurudia mitihani ndilo limechelewesha fedha hizo kuwafikia.

Imani yangu hilo suala litamalizika na hizo saa 72 walizozitoa hazitafika huko. Mchana huu wanakutana na baada ya hapo tutawajulisha,” amesema