Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 9:41 pm

NEWS: SEREKALI YATOA FURSA TENA KWA WAOMBAJI WA VYUO

Dodoma. Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia nchini imeliagiza Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (Nacte) kufungua dirisha dogo la usajili kuanzia leo Jumamosi Septemba 7 hadi 21, 2019 ili kujaza nafasi za masomo zilizopo kwenye vyuo na taasisi mbalimbali


Akizungumza leo Jumamosi Septemba 7, 2019 jijini Dodoma, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk Leonard Akwilapo amewataka wanafunzi kufanya uchaguzi kwa umakini ili wasije kukosa tena nafasi za kujiunga na mafunzo kwa mwaka wa masomo 2019/2020.



“Wizara ya Sayansi na Teknolojia inapenda kutoa rai kwa wahitimu wa kidato cha nne na sita walio na sifa za kujiunga na mafunzo mbalimbali kutumia fursa hii kufanya maombi ya udahili,” amesema.


Dk Akwilapo amesema waombaji 11,028 walichaguliwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na Nacte na kupangiwa vyuo vya mafunzo ya ualimu katika ngazi ya astashahada na stashahada katika vyuo vya Serikali vya ualimu.

Aidha, amesema waombaji 5,309 wamechaguliwa kujiunga na vyuo mbalimbali vya afya vya Serikali.