- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SEREKALI YASHINDWA KULETA MASHAHIDI KESI YA HALIMA MDEE
Dar es Salaam. Hakimu Mkazi mkuu wa Mahakama ya Kisutu, jijini Dar es salaam Thomas Simba ameutaka upande wa mashtaka kuwaleta mahakamani shahidi wa kesi ya kutoa lugha chafu dhidi ya Rais wa Tanzania, John Magufuli inayomkabili mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee.
Amesema kutoletwa kwa shahidi kunampa wakati mgumu kuandika ripoti zake za kesi hiyo inayomkabili kiongozi huyo wa kinamama Chadema (BAWACHA).
Hakimu simba ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Octoba 3, 2019 baada ya wakili wa Serikali, Wankyo Simon kuieleza mahakama hiyo kuwa shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kuendelea na ushahidi lakini shahidi waliokuwa wakimtegemea anaumwa na ameaga kuwa anakwenda Hospitali.
"Shahidi alikuja hapa mahakamani kwa kujikongoja hivyo ameniaga ameenda hospitali, naiomba mahakama hii ipange tarehe nyingine," amedai Simon.
Katika maelezo yake hakimu Simba amesema ameahirisha shauri hilo kwa muda mrefu na inamsumbua katika ripoti zake, kuutaka upande wa mashtaka kuhakikisha shauri hilo litakapotajwa tena mahakamani wawe na shahidi.
Hakikisheni upande wa mashtaka shauri hili linaendelea sio lazima awe shahidi mmoja mwingine akiumwa aje mwingine,” amesema hakimu Simba.
Wakili wa utetezi, Peter Kibatala amedai upande wa mashtaka unadai shahidi anaumwa bila kutoa vielelezo vinavyoonyesha kama kweli anaumwa.
Kibatala amedai anachofahamu ni kuwa shahidi huyo haumwi alikuwepo mahakamani hapo na walipomuuliza aliwaeleza anaenda kutoa ushahidi sehemu nyingine.
Baada ya maelezo hayo Hakimu Simba ameahirisha shauri hilo hadi Oktoba 29 na 30, 2019 itakapokuja kwa ajili ya kusikiliza ushahidi.
Katika kesi ya msingi inadaiwa kuwa Julai 3, 2017 katika ofisi za makao makuu ya Chadema zilizopo mtaa wa Ufipa wilayani Kinondoni, Halima alitamka maneno dhidi ya Rais Magufuli kuwa, “anaongea hovyo, anatakiwa afungwe breki,” kitendo kinachodaiwa kuwa ni kumdhalilisha Rais na kusababisha uvunjifu wa amani.