Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 10:22 pm

NEWS: SEREKALI YASEMA WAMEFANIKIWA KUZIMA LAINI LAKI 975

Dar es Salaam. Mamlaka ya Mawasilino nchini Tanzania (TCRA) imesema kuwa imefanikiwa kuzima laini za Simu 975,041 hii ni mpaka jana saa nne usiku.

Akizungumza na Shirika la Habari la Tanzania TBC leo Asubuhi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), James Kilaba amesema uzimaji wa laini za simu ambazo hazijasajiliwa kwa alama za vidole unafanyika kwa awamu kuanzia jana Jumatatu Januari 20, 2020 ili kuondoa usumbufu.

Amesema kundi la kwanza waliozimiwa laini ni watu 656,091 ambao wana vitambulisho vya Taifa au namba lakini hawajasajili laini zao.

Kilaba amesema kundi la pili ni watu 318,950 waliosajili laini zao kwa kitambulisho cha Taifa kabla ya kuanza mfumo wa kusajili kwa alama za kidole.

“Hawa wote hawana sababu ya kutozimiwa laini zao leo, uzimaji huu hatutaki kumnyang’anya mtu laini yake ambayo ameizoea ila tutaisitisha kutoa na kupokea huduma. Hivyo simu yake itapokea ujumbe mfupi tu ambao utakuwa unamkumbusha usajili” amesema Kilaba akibainisha kuwa usajili wa laini za simu hauna kikomo

Ameongeza, “tunazima kidogo kwa sababu ya mambo ya kitaalamu, hauwezi ukazima laini milioni tano au 10 kwa mara moja.”

“Tunahitaji warudi, tukiwazimia tunategemea kesho watarudi kwenye foleni za kuhuisha laini zao kwa hiyo wakienda wengi zaidi hawatapata huduma kama ambavyo walijaa juzi na jana na leo mpaka mifumo ya Nida inaelemewa.”

Amesisitiza kuwa watafanya kistaarabu na kiufundi uzimaji laini ili mifumo isielemewe kwenye usajili.