Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 8:38 pm

NEWS: SEREKALI YASEMA TRA INAUPUNGUFU YA WAFANYAKAZI 2,249

Dodoma. Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji amesema kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ina upungufu wa watumishi 2,249 ili kufikia idadi ya watumishi 7000 wanaohitajika nchi nzima idadi hiyo ni sawa na Robo ya Idadi nzima.

Kauli hiyo ameitoa leo bungeni Ijumaa Septemba 13, 2019 wakati akijibu swali la msingi la mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Tunza Malapo aliyehoji ni watumishi wangapi wanahitajika TRA ili mamlaka hiyo iweze kufanya kazi zake kwa ufanisi.

Dk Kijaji amesema kwa sasa TRA ina waajiriwa 4,751 ambao wanaendelea na kazi na wakati wowote wataajiri wafanyakazi 150 na wataendelea kuajiri kadri uwezo utakavyoruhusu.

Dk Kijali amesema upungufu uliopo ni wa asilimia 28 na aliahidi kumpatia mbunge mchanganuo wa mahitaji yote kwa waliopo kazini na wanaohitajika.