- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SEREKALI YASEMA SHILINGI YA TANZANIA YAIMARIKA
Dodoma: Serekali ya Tanzania imesema kuwa Thamani ya shilingi ya Tanzania imeendelea kuimarika na katika kipindi kinachoishia Aprili 2019, Dola moja ya Marekani ilibadilishwa kwa wastani wa Sh2,300.9 ikilinganishwa na Sh2,270.3 katika kipindi kama hicho mwaka 2018.
Taatifa hiyo ya Hali ya Uchumi nchini imetolewa leo Alhamisi Juni 13, 2019 na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango wakati akiwasilisha bungeni jijini Dodoma taarifa ya hali ya uchumi wa Taifa mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2019/2020.
“Sababu nyingine ni baadhi ya viwanda kuzalisha bidhaa ambazo awali zilikuwa zikiagizwa kwa wingi kutoka nje ikiwemo vigae na marumaru,” amesema Dk Mpango.
Mpango amesema Utulivu katika mwenendo wa thamani ya shilingi umetokana na utekelezaji wa sera ya fedha, usimamizi madhubuti wa mapato na matumizi ya Serikali, matumizi ya gesi asilimia badala ya mafuta na kuzalisha umeme.