- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SEREKALI YARUDISHA KODI TAULO ZA KIKE
Dar es Salaam. Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amependekeza kufutwa kwa msamaha wa kodi ya ongezeko la thamani iliokuwa kwenye taulo za kike baada ya Waingizaji na wasambazaji wa bidhaa hizo kutoshusha bei baada ya Kutolewa kodi mwaka jana.
Akiwasilisha makadirio na mapato ya Bajeti ya Serikali leo Alhamisi Juni 13, 2019 bungeni jijini Dodoma, Waziri Mpango ametoa sababu ya mapendekezo hayo kuwa msamaha uliowekwa haujawezesha kupatikana kwa bidhaa hiyo muhimu kwa bei nafuu kwa walengwa na badala yake unawanufaisha wafanyabiashara.
“Wakati Serikali ilipoweka msamaha huu ilitarajia kwamba wazalishaji wa taulo za kike wataziuza kwa bei nafuu badala ya kusamehewa,” amesema Waziri Mpango