- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SEREKALI YAPOKEA MKOPO WA SH. 414 BIL KUJENGA RING ROAD DODOMA
Serekali ya Tanzania imepokea mkopo wa dola za kimarekani $180m sawa na Tsh. bilioni 414 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB kwa ajili ya ujenzi wa barabara za pete (ring road) ama mzunguko kwa kiwango cha lami umbali wa kilometa 110.2 na uboreshaji wa miundombinu katika maeneo ya Jiji la Dodoma, Makao Makuu ya nchi ya Tanzania.
Hatua hiyo imefikiwa leo Agosti 19, 2019 Baada ya serekali kupitia Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James kutiliana saini ya makubaliano na Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB, Bw. Alex Mubiru wa kutoa mkopo huo wenye masharti nafuu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa pili kulia) na Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB, Bw. Alex Mubiru wakitia saini makubaliano ya mkataba wa mkopo