- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SEREKALI YAPIGA MARUFUKU MIKUTANO YA MAALIM SEIF
Unguja. Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, Hamad Masauni amemuagiza Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro kuwaondoa makamanda wawili wa polisi kisiwani Pemba kwa kushindwa kuzuia mikutano ya mshauri wa chama cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad.
Masauni ametoa agizo hilo leo Alhamisi Desemba 12, 2019 katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Unguja.
Amesema kwa muda mrefu kisiwa cha Pemba kimekuwa na matukio yasioridhisha jambo linaloashiria kuwa wameshindwa kazi.
Makamanda hao ni Hassan Nassir Ally wa Mkoa wa Kusini Pemba na Sheikhan Mohamed Sheikhan wa Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Akitoa mfano wa matukio hayo, Masauni amesema Maalim Seif anafanya mikutano kila kona huku ikijulikana kuwa imezuiwa.
Amesema sababu nyingine ni kutojengwa nyumba za polisi kisiwani humo licha ya Serikali kutoa maagizo.