- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SEREKALI YAPIGA MARUFUKU KUSAMBAZA PICHA ZA AJALI
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni ameviagiza Vyombo vya Dola nchini kuwashughulikia wale wote wenye tabia ya kusambaza picha za marehemu baada ya kutokea kwa Ajali.
Masauni ameyasema hayo Leo Jumatatu Agosti 12 baada ya Swala ya Eid iliyofanyika katika Msikiti Mkuu mjini Morogoro.
“Si vyema kuanza kutumia janga hili la kitaifa lililotukuta… kwa dhamira ya kudhalilisha watu wengine.”- Kauli ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
Masauni ameyasema haya mara baada ya kutokea kwa Ajali ya lori la Futa nchini na watu 71 kupoteza maisha katika eneo la Msamnvu mkoani Morogoro.
Jana taifa liliwazika watu 71 waliopoteza maisha katika mripuko huo.
Maafisa wa usalama waliwazika marehemu hao ambao miili yao iliwekwa katika majeneza meupe, baada ya sala fupi iliyoongozwa na viongozi wa dini za kiislamu na kikristo.
Rais wa nchi hiyo, John Pombe Magufuli ametangaza siku tatu za msiba wa kitaifa. Walioshuhudia tukio hilo baya walisema lori hilo lilipinduka wakati dereva wake alipokuwa akijaribu kumkwepa mwendesha bodaboda, na kundi kubwa la watu walifika huko kuchota mafuta yaliyokuwa yakivuja.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro amesema mripuko ulisababishwa na cheche wakati mporaji mmoja alipokuwa akijaribu kuchomoa bateri ya lori hilo. Matukio kama haya hutokea mara kwa mara katika nchi nyingi za kiafrika.