Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 5:37 am

NEWS: SEREKALI YAPIGA MARUFUKU KUSAFIRISHA WANYAMA HAI NJEE YA NCHI

Dodoma: Wizari ya Maliasili na Utalii, imesema kuwa kuanzia sasa hivi kwa maana ya leo Serikali ya Tanzania haitaruhusu usafirishaji wa wanyama hai nje ya nchi tena.

Kauli hiyo ya Serekali imetolewa Leo Ijumaa Februari 8, 2019 Bungeni Jijini Dodoma na Waziri mwenye dhamana Dk Hamisi Kigwangalla wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Muheza (CCM), Balozi Adadi Rajabu.

Mbunge huyo alitaka kujua Mei, 2019 Watanzania wataanza kusafirisha wanyama hai ikiwemo akina mama wa kijiji cha Fanusi wilaya ya Muheza ambao husafirisha vipepeo. "Niseme wazi kuanzia sasa hatutaruhusu wanyama hai kusafirishwa kwenda nje ya nchi na wale waliokuwa wanafanya biashara hiyo watafute njia nyingine," amesema Kigwangalla.

Kauli hiyo ya Waziri Kigwangalla imefuta agizo la Wizara hiyo ambayo iliweka zuio la miaka mitatu mpaka Mei, 2019 ilikuwa ndiyo mwisho wa zuio hilo.