- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SEREKALI YAPIGA MARUFUKU KUCHUKUA FOMU KWA MBWEBWE
Dodoma. Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Seleman Jafo amevionya Vyama vya siasa kuacha tabia ya kuchukua fomu kwa mbwembwe na shamrashara zenye viashiria vya kampeni kwa wagombea wa nafasi za wenyeviti wa vijiji, mitaa na vitongoji kama sehemu ya kampeni na badala yake wasubirie mpaka muda wa kampeni utakapotangazwa
Waziri Jafo ametoa onyo hilo leo Jumatatu Oktoba 28, 2019 katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu utoaji na uchukuaji fomu kuanzia kesho.
Waziri huyo amesema fomu kwa wagombea hao zitaanza kutolewa kesho Oktoba 29 hadi Novemba 4, 2019 lakini akasema mbwembwe zitapelekea watu kufanya kampeni wakati muda bado.
Waziri amesema shamrashamra zitaashiria kuwa kampeni zimeanza wakati muda wa kampeni haujawadia.
"Kusindikizwa si jambo baya lakini kuwa na shamrashamra ni wazi kuwa watakuwa wanafanya kampeni, hilo halitakubalika kamwe, twendeni kwa utulivu ili tuvuke salama," amesema Jafo.
Pia ameviagiza vyama vya siasa kuwa makini zaidi na ujazaji fomu za wagombea wao ili kuepuka malalamiko ambayo yamekuwa yakijitokeza katika maeneo mengi.
Kwa mujibu wa Jafo, baadhi ya viongozi wanashindwa kuwashauri na kuwasaidia wagombea wao ambao mwisho wa siku hujikuta wamekosea lakini kwa kuwa muda wanao wa kutosha ni vema wakajipanga.