- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SEREKALI YAPANGA KUJENGA HOSPITALI YA KANDA YA ZIWA CHATO
Dodoma. Serikali ya Tanzania imesama inampango wa kujenga Hospitali ya Kanda ya ziwa wilayani Chato Mkoani Geita itakayohudumia wakazi wote waishio Mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Akiwasilisha taarifa yake kwa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii leo Jumatatu Januari 20, 2020, Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Ummy Mwalimu amesema Serikali inatarajia kujenga hospitali hiyo kutokana na idadi kubwa ya watu kuwa eneo hilo.
“Tumefanya utafiti na kugundua kuna wagonjwa wengi Kanda ya Ziwa kwa hiyo tunajenga Zonal Hospital (hospitali ya Kanda) Chato,” amesema.
Amesema kuwa sababu ya kujenga hospitali hiyo Chato ni Mikoa ya kanda ya ziwa kuwa na watu zaidi milioni 15.
Baada ya Waziri Ummy kueleza hayo, baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CCM), Peter Serukamba walicheka.